Thursday, September 3, 2009

WALIMU WATAKIWA KUBADILIKA

WALIMU Mkoani Shinyanga wametakiwa kuipenda na kuiheshimu kazi yao ikiwa ni pamoja na kubadilika katika utendaji wa kazi zao ili kuondokana na aibu ambayo huikumba mkoa huo kwa kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa kwa shule zao.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni katika eneo la Mwanhuzi Wilaya ya Meatu na Kaimi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,Bi.Georgia Machumu wakati akifungua mafunzo ya walimu wa shule za msingi nchini.
Bi.Machumu alisema kuwa wakati umefika kwa kila mwalimu shuleni kuhakikisha anabadilika na kutambuwa wajibu wake na dhamana kubwa katika taifa hili kwa kuondoa adui mjinga.

1 comment:

  1. NA SERIKALI NA YENYEWE INACHANGIA, HUWEZI UKAMPELEKA MTU AKAFANYE KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU HALAFU UKATARAJIA UFANISI WA KAZI, WABORESHE MIUNDO MBINU MUHIMU KWANZA KABLA YA KUANZA KUWALAUMU WALIMU.

    ReplyDelete