Friday, September 11, 2009

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI ASHIKILIWA KWA KUVUJISHA MTIHANI

MWALIMU Mkuu katika shule Msingi Kiziko wilayani Mkuranga,Silvester Undole(48)ameunganishwa na walimu wengine wawili wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa taifa wa darasa la saba uliomalizika juzi.
Mkamanda wa polisi mkoa wa Pwani,Absalom Mwakyomo,alisema Undole ambaye alikuwa msimamizi wa mtihani katika shule ya msingi Lupondo,alikamatwa jana baada yakirudisha karatasi pungufu za mitihani hiyo.
"Mwalimu huyu anadaiwa kutoa karatasi za maswali kwa walimu wawili tunaowashikilia wa Lupondo ambao waligawa majibu kwa wanafunzi hao".
Alisema upelelezi wa awali ulibaaini kuwa Undole alikabidhiwa karatasi hizo 32 lakini alirudisha 31 kabla ya kukamatwa kwake.
Alisema mtuhumiwa huyo na watuhumiwa wenzake wawili ambao ni Hamis Katundu (51)na Musa Mayotela(49)walitarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Hajati Amina Said alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea

No comments:

Post a Comment