DAR ES SALAAM,
Walimu nchini watakiwa kujenga tabia ya kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi, kiuchumi, na kiutamaduni kwa vile kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuboresha maisha yao pamoja na jamii inayowazunguka.
Wito huo umetolewa na leo na Mkurugenzi Mkuu wa wa kampuni yakuchapisha vitabu na magazeti ya Bussiness Printers Limited Bwana Rashidi Mbuguni alipokua akifungua semina ya siku moja inayolenga kuwawezesha walimu wa masomo ya hesabu na biashara kwa ngazi ya Sekondari kufundisha kwa vitendo.
Bwana Mbuguni amesema kuwa umefika wakati ambao walimu nchini wanatakiwa watumie vitendo zaidi ya maelezo ikiwa ni pamoja na kuandaa vitabu vya masomo wao wenyewe badala ya kutegemea vitabu kutoka nje ya nchi kwa vile haviendani sana na mazingira ya kitanzania.
Kwa upande wao walimu wa somo la hesabu Mkoani Dar es salaam,wamesema kuwa ni muda mrefu wamekuwa wakioomba Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuwaruhusu kuandaa vitabu vyao kwa vile vitabu vingi wanavyotumia vina makosa mengi.
Semina hiyo ya siku moja imedhaminiwa na kampuni ya Bussiness Printers Limited na imeanza kwa mkoa wa Dar es salaam na baadae kuendelea mikoa yote nchini ambapo kampuni hiyo imetoa udhamini wa uchapishji wa vitabu kwa masomo ya hesabu na biashara.
Friday, September 18, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment