Friday, August 7, 2009

MSWADA WA SHERIA WA HAKI ZA WATOTO KWA MWAKA 2009

Na:Malela Kassim

Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na watoto,Bibi Margareth Simwanza Sitta ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuunga mkono hoja inayoitaka Serikali kipitisha sheria inayowahusu watoto wa kike nchini kuendelea na masomo baada ya kujifungua kufuatia kupewa mimba wakiwa bado wanaendelea na masomo.
Akitolea mfano wa nchi za Zambia,Malawi na Zanzibar ambazo zimepitisha na kutumia sheria hiyo Bibi Sitta amesema kuwa nchi hizo zinafanya vizuri kielimu na pia zinawapa watoto wa kike haki ya kupata elimu ambayo ni haki ya kila mtoto ulimwenguni pote.

Kwa upande wake mjumbe wa kushugulikia haki za watoto Nchini Ghana Bibi Agnes Akosua Aidoo ameiomba Serikali ya Tanzania kuhakikisha inatoa bure vyeti vya kuzaliwa kwa kuwa hiyo ni haki ya kwanza ambayo mtoto anatakiwa apewe mara baada ya kuzaliwa.

Mswada huo mpya wa haki za watoto unalenga kuweka Mashirika maalumu kwa ajili ya kuboresha,kuhifadhi na kulinda haki za watoto ili kuhifadhi matakwa ya mikataba ya kimataifa kuhusu haki ya mtoto

No comments:

Post a Comment