Tuesday, August 18, 2009

Bi.Ngoye ANENA NA WAZAZI

MBUNGE wa viti maalumu(ccm)kutoka mkoa wa Mbeya Bi.Hilda Ngoye ametaka wanafunzi wanaopeana mimba wakiwa shuleni wote wafukuzwe kwa pamoja ili kujenga nidhamu kwa vijana wengine.
Hayo yamezungumzwa wakati akihutubia wazazi na wanafunzi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya shule ya sekondari ya wazazi META ya jijini Mbeya jumamosi Agost 15 mwaka huu.
Bi.Ngoye amesema kuwa kukithiri kwa vitendo vya ujauzito katika shule za msingi na sekondari husababishwa na jinsia zote hivyo inapobainika aliyempa mwanafunzi mimba ni mwanafunzi mwenzie naye anapaswa kuwajibika
"Wanafunzi wa kike wanaopewa mimba na wale wanaosababisha mimba wote wanatakiwa kutimuliwa.........hii itakuwa njia mbadala ya kukomesha wimbi la mimba baina ya wanafunzi kwa wanafunzi".alisema Bi.Ngoye

No comments:

Post a Comment