Monday, December 6, 2010

MATOKEO YA MITIHANI DARASA LA SABA YATANGAZWA

Na.Joyce Mtavangu.
Njombe
Imeelezwa kuwa hali ya utoro ambayo imekithiri miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi ndio chanzo cha kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi wanao hitimu darasa la saba katika wilaya ya njombe mkoani Iringa.

Hayo yamesemwa na afisa elimu wilaya ya njombe Bw Bartazar Kessy. alipokuwa akizungumza Ofisini kwake ambapo amesema kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kimeshuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu,ukilinganisha na msongamano pamoja na utoro.

Aidha katika kupambana na adha ya kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao, Serikali imeweka mkakati wa kutoa vyakula mashuleni ili kukabiliana na tatizo la utoro ambalo ndiyo chanzo cha wanafunzi wengi kufeli.Hata hivyo ameongeza kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeshuka kwa asilimia 0.29 ukilinganisha na mwaka jana ambapo kiwango cha kufaulu kilikuwa ni asilimia 66.27 tofauti na mwaka huu ambapo kiwango cha wanafunzi waliofaulu ni asilimia 65.5.

Pia bwana Kessy amesema idadi ya wanafunzi waliofanya mtihani ni 9100 kwa wilaya nzima,ambapo idadi ya waliojiandikisha ni 9210,huku waliofaulu ni 5969.Bwana Kessy amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu ikiwa ni pamoja na kufuatilia mwenendo wa taaluma na kusaidiana na kamati ya shule kuimarisha mazingira ya shule.

1 comment:

  1. alaaaaaaaaa, eboooooooooooo, pumbaaaaaaavuuuuuuuuu.....wazazi wao wako wapi?...kudadadeki mitoto kama hiyo unairudiha anaanza upya darasa la kwanza nyoooooooooo

    ReplyDelete