Friday, September 18, 2009

DAR ES SALAAM,

Walimu nchini watakiwa kujenga tabia ya kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi, kiuchumi, na kiutamaduni kwa vile kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuboresha maisha yao pamoja na jamii inayowazunguka.

Wito huo umetolewa na leo na Mkurugenzi Mkuu wa wa kampuni yakuchapisha vitabu na magazeti ya Bussiness Printers Limited Bwana Rashidi Mbuguni alipokua akifungua semina ya siku moja inayolenga kuwawezesha walimu wa masomo ya hesabu na biashara kwa ngazi ya Sekondari kufundisha kwa vitendo.


Bwana Mbuguni amesema kuwa umefika wakati ambao walimu nchini wanatakiwa watumie vitendo zaidi ya maelezo ikiwa ni pamoja na kuandaa vitabu vya masomo wao wenyewe badala ya kutegemea vitabu kutoka nje ya nchi kwa vile haviendani sana na mazingira ya kitanzania.

Kwa upande wao walimu wa somo la hesabu Mkoani Dar es salaam,wamesema kuwa ni muda mrefu wamekuwa wakioomba Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuwaruhusu kuandaa vitabu vyao kwa vile vitabu vingi wanavyotumia vina makosa mengi.

Semina hiyo ya siku moja imedhaminiwa na kampuni ya Bussiness Printers Limited na imeanza kwa mkoa wa Dar es salaam na baadae kuendelea mikoa yote nchini ambapo kampuni hiyo imetoa udhamini wa uchapishji wa vitabu kwa masomo ya hesabu na biashara.
DAR ES SALAAM,

Bwana Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa rais wa zamani Tanzania Hayati Mwl. Julius Nyerere pamoja na Jaffar Amini ambaye ni mtoto wa raisi wa zamani wa Uganda Iddi Amin kwa pamoja wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za hisani kuwasaidia watoto yatima wanaolelewa na asasi isiyo ya kiserikali ya Community Alive iliyoko mjini Musoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo Bwana Madaraka Nyerere amesema hatua hiyo pia inalenga kumuenzi baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo kwa pamoja wanatarajia kuanza kupanda mlima huo Octoba 29 hadi Novemba 6 mwaka huu.

Bwana Madaraka amewaomba wananchi mbalimbali kuchangia asasi hiyo ili kufanikisha lengo lake la kuwasaidia watoto hao ambao wameachwa na wazazi wao kutokana na ugonjwa wa Ukimwi kupitia namba ya akaunti 064-6000246 kwenye benki ya Barclays tawi la Musoma kupitia jina la Community Alive.

Hii ni mara ya pili kwa Bwana Madaraka kuchangisha fedha za hisani ambapo mwaka jana alifanikiwa kuchagisha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 22 zilizowezesha ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari ya wasichana ya Mtemi Edward Wanzagi iliyopo mkoani Mara.

Hayati Mwalimu Nyerere na Iddi Amini walikuwa na tofauti kubwa za kisiasa kitu kilichopelekea kuvunjika kwa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 na chanzo cha vita vya Kagera mwaka 1979.

JAMII YAHIMIZWA KUSAIDIA YATIMA ELIMU

TAASISI na kampuni zimehimizwa kusaidia watoto yatimana wanaoishi katika mazingira magumu,ili waweze kutimiza ndoto zao maishani.
Mwiti huo ulitolewa jana na Dar es salaam na Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima cha Mkakuya Ophans na Vulnerable Children Center,Cecilia Nasoro,wakati akipokea msaada wa futari kutoka kampuni ya simu Tanzania(TTCL).
Kampuni hiyo ilitoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh.milioni tano kwa vituo vinne vya kulelea watoto.Mbali na Mkakuya vingine ni Msongora Ophans Trust Fund, vilichoko Mbagala,Mama Teresa na Nuruhud Madrasat vya Mburahati,Dar es salaam
Wakati akipokea msaada huo,Nasoro alisema misaada ya watoto hao isiishie kutoa vyakula na mambo mengine,isipokuwa sasa kampuni,taasisi na jamii zijizatiti kutoa udhamini wa elimu na ajira salama kwa watoto hao.

Friday, September 11, 2009

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI ASHIKILIWA KWA KUVUJISHA MTIHANI

MWALIMU Mkuu katika shule Msingi Kiziko wilayani Mkuranga,Silvester Undole(48)ameunganishwa na walimu wengine wawili wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa taifa wa darasa la saba uliomalizika juzi.
Mkamanda wa polisi mkoa wa Pwani,Absalom Mwakyomo,alisema Undole ambaye alikuwa msimamizi wa mtihani katika shule ya msingi Lupondo,alikamatwa jana baada yakirudisha karatasi pungufu za mitihani hiyo.
"Mwalimu huyu anadaiwa kutoa karatasi za maswali kwa walimu wawili tunaowashikilia wa Lupondo ambao waligawa majibu kwa wanafunzi hao".
Alisema upelelezi wa awali ulibaaini kuwa Undole alikabidhiwa karatasi hizo 32 lakini alirudisha 31 kabla ya kukamatwa kwake.
Alisema mtuhumiwa huyo na watuhumiwa wenzake wawili ambao ni Hamis Katundu (51)na Musa Mayotela(49)walitarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mkuranga kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Hajati Amina Said alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea

Saturday, September 5, 2009

WANAFUNZI KUJIPELEKA WENYEWE POLISI

MKUU wa mkoa wa Pwani,Bi.Amina saidi,amewataka wanafunzi wa kike ambao watashindwa kuwataja wanaume wanaosababisha ujauzito,kujipeleka wenyewe polisi.
Bibi Amina,ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika shule ya wasichana ya Tumbi inayomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha,mkoani Pwani
Bibi Amina amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike hawapo tayari kuwataja wanaume wanaowasababishia mimba hizo,haliambayo licha ya kuwakatisha masomo,laikini pia inasababisha Serikali kushindwa kuwachukulia hatua watuhumiwa hao.

Friday, September 4, 2009

WATOTO YATIMA WASAIDIWE

WAMILIKI wa shule binafsi na mashirika ya kidini nchini wameshauriwa kutenga nasafi za upendeleo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwanusuru katika majanga mbalimbali.
Akizungumza jana mjini Dodoma,Mkurugenzi wa Rhema Academy Pre and Primary School,Neema Majule alisema kuwa jukumu la kuwalea watoto hao ni la kila Mtanzania,hivyo inatakiwa kujitolea kwa hali na mali.
"Licha ya shule zetu kuwa za kibiashara,mwito wangu kwa wamiliki ni kuwa tutenge hata nafasi kidogo ili tuweze kuwasaidia na hawa watoto"alisema.
Alisema shule hiyo ina wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira magumu zaidi ya 20 ambao wanasoma bure wakigharamiwa ada,chakula,mavazi,na usafiri

Thursday, September 3, 2009

WALIMU WATAKIWA KUBADILIKA

WALIMU Mkoani Shinyanga wametakiwa kuipenda na kuiheshimu kazi yao ikiwa ni pamoja na kubadilika katika utendaji wa kazi zao ili kuondokana na aibu ambayo huikumba mkoa huo kwa kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa kwa shule zao.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni katika eneo la Mwanhuzi Wilaya ya Meatu na Kaimi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu,Bi.Georgia Machumu wakati akifungua mafunzo ya walimu wa shule za msingi nchini.
Bi.Machumu alisema kuwa wakati umefika kwa kila mwalimu shuleni kuhakikisha anabadilika na kutambuwa wajibu wake na dhamana kubwa katika taifa hili kwa kuondoa adui mjinga.