Saturday, August 29, 2009

KORTINI KWA MAUWAJI IDODI

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu shule ya sekondari Idodi,mkoani Iringa Erick Mnyali(16),anayedaiwa kusababisha moto bweni la wasichana la shule hiyo na kuua wanafunzi 12,amefikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Iringa kwa makosa 12 ya kuua bila kukusudia.
Mtuhumiwa huyo alipandishwa katika mahakama hiyo majira ya saa 8.30 alasiri jana na kesi yake inasomwa kuwa mauaji namba 29 ya mwaka 2009.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Geofrey Mhini,Mwendesha mashitaka Mratibu wa Polisi,Mwenda alidai kuwa mtuhumiwa alitenda makosa hayo Agost 23,mwaka huu.

Friday, August 28, 2009

JELA MIAKA 30 KWA KUNAJISI

MKAZI wa Buguruni Kisiwani Deogratias Joseph Lyimo(27) amehukumiwa miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka.

Kabla hakimu Janeth kinyage wa mahakama ya wilaya ya Ilala kutoa hukumu hiyo,Mwendesha mashitaka wa polisi,Inspekta Mussa Gumbo,aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili kukomesha vitendo kama hivyo katika jamii.

Hakimu Kinyange amesema kuwa kutokana na maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo na pande zote mbili,mahakama imemuhukumu mshitakiwa kutumikia kifungo miaka hiyo ili iwe fundisho kwa wengine.

Mh.MAHIZA AWAWAKIA WALIMU

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Bi.Mwantumu Mahiza amesema ole wake mwalimu atakayebainika kufungia vitabu katika kabati lake badala ya kuwagawia wanafunzi wajisomee na kujifunza mambo mbalimbali.
Alitoa onyo hilo kwa walimu wa sekondari na msingi hivi karibuni,baada ya kutembelea shule mbalimbali za msingi na sekondarikatika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa na kugundua kuwa baadhi ya walimu wanalalamikia upungufu mkubwa wa vitabu...Bi.Mahiza alisema ni jambo la ajabu hata majarida mbalimbali yanayotolewa na taasasa mbalimbaliyanayoelezea kuhusu UKIMWI yamefungiwa bila kuwagawia wanafunzi wanaopaswa kuwa na uelewa kuhusu ugonjwa huo.
"Jamani vitabu si mali ya mwalimu bali ni mali ya mwanafunzi hivyo ni lazima vitabu vyote vitoke maofisini na kuwafikia walengwa ambao ni wanafunzi na nasema kuwa agizo hili si kwa Sumbawanga pekee bali ni kwa nchi nzima"alisema Bi.Mahiza

Tuesday, August 18, 2009

Bi.Ngoye ANENA NA WAZAZI

MBUNGE wa viti maalumu(ccm)kutoka mkoa wa Mbeya Bi.Hilda Ngoye ametaka wanafunzi wanaopeana mimba wakiwa shuleni wote wafukuzwe kwa pamoja ili kujenga nidhamu kwa vijana wengine.
Hayo yamezungumzwa wakati akihutubia wazazi na wanafunzi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya shule ya sekondari ya wazazi META ya jijini Mbeya jumamosi Agost 15 mwaka huu.
Bi.Ngoye amesema kuwa kukithiri kwa vitendo vya ujauzito katika shule za msingi na sekondari husababishwa na jinsia zote hivyo inapobainika aliyempa mwanafunzi mimba ni mwanafunzi mwenzie naye anapaswa kuwajibika
"Wanafunzi wa kike wanaopewa mimba na wale wanaosababisha mimba wote wanatakiwa kutimuliwa.........hii itakuwa njia mbadala ya kukomesha wimbi la mimba baina ya wanafunzi kwa wanafunzi".alisema Bi.Ngoye

Thursday, August 13, 2009

MATATANI KWA KUTOMASA NYETI ZA CHEKECHEA

MSHITAKIWA Omary Amiry miaka 40 mkazi wa Mbezi kwa Msuguli amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kujibu mashitaka ya kumshikashika mtoto wa kike wa miaka 6 sehemu zake za siri.

Mbele ya Hakimu Hilda Lyatuu imedaiwa na mwendesha mashitaka Inspeta wa polisi Benedict Nyagabona kuwa,Julai 21 mwaka huu,mshitakiwa kwa makusudi alimshikashika mtoto huyo.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na kesi hiyo itatajwa tena Agosti 26 mwaka huu.

Tuesday, August 11, 2009

WARATIBU ELIMU KATA WATAKIWA KUZUNGUMZA NA WAZAZI

WARATIBU Elimu kata nchini wametakiwa kuwaelimisha wazazi kuhusu uhusiano mzuri kati ya walimu,wasimamizi wa shule na wazazi ili mwalimu awe na mazingira mazuri ya kufanya kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Karatu,Bw.Mathew Sedoyeka wakati akifunga semina ya waratibu elimu kata wa wilaya za Karatu,Ngorongoro na manispa ya Arusha iliyofanyika wilayani humo,

ASKOFU MTOKAMBALI SISITIZA MALEZI BORA

ASKOFU Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblis of God(TAG),Dkt.Barnabas Mtokambali amewasisitiza wazazi kuhusu malezi bora kwa watoto wao ili kujenga jamii yenye maadili mema.

Kiongozi huyo wa dini alisema ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kuwa mtoto wake anapata malezi bora ili kuweza kuwajengea msingi mzuri wa maisha ya badae.

Askofu Mtokambali alisema hayo juzi wakati akihubiri katika kanisa la City Center lililoko jijini Tanga na kuwataka waumuni wa kanisa hilo kudumisha upendo miongoni mwao na waumini wa dini nyingine nchini ili kulinda amani na utulivu iliyopo hapa nchini.

Aliongeza kuwa ni vema waumini wa kanisa hilo wakaendelea kuimarisha upendo na mshikamano uliopo nchini kwa kuwatembelea na kuwasaidia watu walio katika makundi yenye mahitaji maalumu nchini ili nao wazidi kuishi kwa amani mioyoni mwao.

Monday, August 10, 2009

Mwandaaji wa Miss tototo Temeke Jackline Magayane akizungumnza katika shindano la kumsaka Miss tototo mwaka 2009

Fatuma Issa(katikati)akiwa na mshindi wa pili na watatu



Fatuma Issa mshindi wa miss tototo temeke 2009 katika pozi





Miss tototo top 5 katika pozi


Miss tototo wakionyesha shoo ya pamojaMtoto Ashura Omary akipita na vazi la mtoko


Mtoto Fatuma Issa akipita na vazi lake la kutokea



Mtoto Eda Damiani akipita na vazi lake la mtoko




Zaituni Hassani akipita na vazi lake la kutokea


Mtoto Fatuma Issa akiwa katika pozi na vazi la ubunifu
Mtoto Jane Antony akipita na vazi la ubunifu


Mtoto Neema Ally akionyesha vazi lake la ubunifu

Msanii wa kizazi kipya Duly syksi akicheza na watoto katika shindano la kumsaka miss tototo temeke ivi karibuni




Wasanii kutoka wakali Dansa wakionyesha manjonjo wakati wa shindano la miss tototo temeke



Sunday, August 9, 2009

hata sisi jamani tunaweza umiss jamani cheki nilivyo pozi














Friday, August 7, 2009

MSWADA WA SHERIA WA HAKI ZA WATOTO KWA MWAKA 2009

Na:Malela Kassim

Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na watoto,Bibi Margareth Simwanza Sitta ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuunga mkono hoja inayoitaka Serikali kipitisha sheria inayowahusu watoto wa kike nchini kuendelea na masomo baada ya kujifungua kufuatia kupewa mimba wakiwa bado wanaendelea na masomo.
Akitolea mfano wa nchi za Zambia,Malawi na Zanzibar ambazo zimepitisha na kutumia sheria hiyo Bibi Sitta amesema kuwa nchi hizo zinafanya vizuri kielimu na pia zinawapa watoto wa kike haki ya kupata elimu ambayo ni haki ya kila mtoto ulimwenguni pote.

Kwa upande wake mjumbe wa kushugulikia haki za watoto Nchini Ghana Bibi Agnes Akosua Aidoo ameiomba Serikali ya Tanzania kuhakikisha inatoa bure vyeti vya kuzaliwa kwa kuwa hiyo ni haki ya kwanza ambayo mtoto anatakiwa apewe mara baada ya kuzaliwa.

Mswada huo mpya wa haki za watoto unalenga kuweka Mashirika maalumu kwa ajili ya kuboresha,kuhifadhi na kulinda haki za watoto ili kuhifadhi matakwa ya mikataba ya kimataifa kuhusu haki ya mtoto